SERIKALI imesema mradi wa ‘Mama Samia Legal Aid Kampeni’ utakuwa msaada kwa wananchi hasa wanyonge kwani licha ya kutoa elimu kwaajili ya uelewa wa mambo ya kisheria lakini pia utawashughulikia wenye migogoro na kesi mbalimbali hasa zilizokwama kutokana na mifumo ya uendeshaji.
Akizungumza leo kwenye mjadala maalumu unaoendeshwa na Idara ya Habari MAELEZO na kuongozwa na Mkurugenzi wa Idara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, ‘Club House’ Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumaro alisema ndani ya kapu la ‘Mama Samia Legal Aid’ limejumlisha watendaji wote wa masuala ya kisheria nchini kutoka sekta za Umma na Binafsi na kwamba lengo ni kuhakikisha wananchi wote wanapatiwa huduma hiyo.
“Kampeni hii itaanzia Jiji la Dodoma itazinduliwa rasmi Aprili 27, 2023 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambapo baada ya uzinduzi huo tutazunguka mkoa mzima wa Dodoma, tutagusa Vijiji, Vitongoji mpaka Mitaa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.