HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea iliyopo Mkoa wa Ruvuma imeshauriwa kujipanga kuwekeza katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ili waweze kunufaika na fursa za uwepo wa makao makuu ya nchi.
Ushauri huyo ulitolewa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago alipokuwa akiwakaribisha timu ya madiwani ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea waliofanya ziara ya mafunzo jijini hapa.
Naibu Meya Chibago aliwakaribisha jijini Dodoma. “Tunawakaribisha Halmashauri ya Manispaa ya Songea na mikoa yote kuja kuwekeza katika Jiji la Dodoma. Mkurugenzi, wapeni maeneo yaliyopangwa ili waje kuwekeza kwenye viwanda na maeneo mengine watakayopenda. Halmashauri nyingine wameshaanza kuwekeza” alisema Naibu Meya Chibago.
Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji ina sifa mbili. “Halmashauri ya jiji ndiyo sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinapotungwa. Lakini pia ndiyo makao makuu ya nchi” alisema Chibago.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepiga hatua kimaendeleo. “Dodoma niliyokuwa naijua siyo hii ya sasa. Unapoenda nje ya Dodoma, unajua mji unakuwa kwa kasi kubwa, haya ni maendeleo makubwa. Dodoma inapiga hatua kubwa na kuzipita halmashauri nyingine. Ndiyo maana tumeamua kuja kujifunza hapa” alisema DC Mgema.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.