MKOA wa Dodoma umepewa heshima na dhamana ya kuandaa shughuli ya maombolezo rasmi kitaifa yatakayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge ametoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Dodoma kuja kushiriki shughuli hii ya maombolezo ya kitaifa ya mpendwa wetu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Maandalizi ya zoezi la kuaga mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli yanaendelea kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Aidha, Dkt. Mahenge amesema kuwa Wananchi wanakaribishwa kufika ili kusaini vitabu vya maombolezo ambayo imeanza leo katika Uwanja wa Nyerere Square na katika Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa hapa Dodoma.
Mwili wa Hayati Dkt. Magufuli utawasili Uwanja wa Ndege Dodoma Jumapili Machi 21, 2021 saa 10 jioni na kuelekea Ikulu ya Chamwino kupitia barabara za Chako ni chako, barabara ya Nyerere, Round about ya Mkuu wa Mkoa/Jamatini, Bunge, Morena, Bwigiri na kuingia Chamwino Ikulu. Wananchi kwenye maeneo hayo mnaombwa kujitokeza kutoa heshima zenu.
Jumatatu Machi 22, 2021 mwili utaagwa katika Uwanja wa Jamhuri kuanzia saa 12:00 asubuhi na zoezi la kuaga litaisha mara baada ya wananchi kumaliza kuaga.
Miongoni mwa shughuli zitakazofanyika siku hiyo ni pamoja na gwaride la mazishi kutoka Jeshi la Wananchi la Tanzania, dua na sala, salamu za maombolezo na kutoa heshima za mwisho.
Jumanne Machi 23, 2021 saa 12 asubuhi mwili wa Hayati Dkt. Magufuli utatolewa katika hospitali ya Benjamin Mkapa na kusafirishwa kuelekea Zanzibar.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.