Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jaii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekutana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na kujadili namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona (COVID-19) nchini.
Katika kikao hicho, Waziri Ummy Mwalimu ameshukuru baraza hilo kwa kushirikiana na sekta ya Afya katika mapambano ya ugonjwa huo. "Mchngo wa sekta binafsi mkiwamo nyie wafanyabiashara ni muhuimu kwani mtaleta manufaa makubwa katika mapambano haya" amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa TPSF, Bi. Angelina Ngalula amesema watahakikisha vifaa kinga vinavyohitajika vinasambazwa kila mkoa na wilaya nchini ili kukabiliana na ugonjwa wa homa ya Corona.
Katika kuhakikisha kwamba sekta hiyo inakabiliana na maambukizi ya homa ya Corona, TPSF imekubaliana na wamiliki nchini kuapatika madereva na wasaidizi wao vifaa kinga. "Sisi kama sekta binafsi tutahakikisha kwamba tunalinda ajira za watumishi wetu kwa gharama zote," amesema Bi. Ngalula.
Naye Mwenyekiti wa TPSF inayosimamaia Jitihada za kukabiliana na maambukizi ya Homa ya Corona, Bw. Abdulsamad Abdulrahim amesema sekta binafsi imebaisisha maeneo 26 katika mkoa wa Dar es Salaam ambayo ni hatarishi kwa maambukizi ya homa ya Corona na kwamba vijana wanaelekea mikoani kwa ajili ya kubaini maeneo mengine.
Bw. Abdulrahim amesema katika upande wa elimu ya afya nyakati za dharura na majanga, wamewasiliana na kampui za simu na kwamba tayari zimeanza kusambaza ujumbe kuhusu elimu ya kujikinga na maambuziki ya homa ya Corona. "Tumewatafuta wadau wanaomiliki mabango barabarani nchi nzima na wameweka ujumbe wa kukambiliana na maambukizi ya ugonjwa huu. Mheshimiwa Waziri hivi tunavyozungumza, tayari jumbe mbalimbali zimeshawekwa kwenye mabango ya barabarani" amesema Bw. Abdulrahim.
Mwenyekiti wa TPSF, Bi. Angelina Ngalula aliyeshiriki katika kikao na Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jaii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa TPSF, Bi. Angelina Ngalula (kushoto) na Mwenyekiti wa TPSF inayesimamia jitihada za kukabiliana na maambukizi ya Homa ya Corona, Bw. Abdulsamad Abdulrahim (kulia) walipokuwana kujadiliana namna ya kukabiliana na maambukizi ya virusi ya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.
Chanzo: Wizara_afyatz (Instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.