Serikali imewasilisha bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21 katika hotuba iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika Hotuba hiyo Waziri Mpango alitaja mafanikio yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Moja ya mafanikio hayo ni kuhamishia shughuli za Serikali Makao Makuu Dodoma ameainisha Dkt. Mpango.
Akifafanua zaidi Dkt. Mpango amesema, Serikali imefanikisha ndoto ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuhamishia Makao Makuu ya Serikali jijini Dodoma kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi ambapo jumla ya watumishi 8,883 wa Wizara na Taasisi za Serikali wamehamishiwa Makao Makuu ya Serikali, Dodoma na ujenzi wa ofisi 23 za Wizara katika mji wa Serikali, Mtumba umekamilika, ikijumuisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Chanzo: www.bunge.go.tz
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.