MSEMAJI Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amefanya mkutano na kuwaeleza waandishi wa Habari kuhusu ujio wa viongozi wa mataifa mbalimbali kushiriki kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Machi 22, 2021 Jijini Dodoma.
Takribani Marais 10 wanatarajiwa kuhudhuria maombolezo ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli yatakayofanyika kesho (Machi 22, 2021) kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Amewataja marais waliothibitisha kushiriki kuwa ni Uhuru Kenyata (Kenya), Lazarus Chikwera (Malawi), Azali Assoumani (Comoro), Filipe Nyusi (Msumbiji), Emmerson Mnangagwa (Zimbabwe), Edgar Rungu (Zambia), Hage Geingob (Namibia), Mokgweetsi Masisi (Botswana), Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini) na Felix Tshisekedi (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC).
Baadhi ya Marais ambao hawatohudhuria, wametuma wawakilishi wao.
Marais watakaohudhuria ni pamoja na Rais wa Kenya, Malawi, Commoro, Msumbiji, Zambia, Namibia, Botswana, Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mataifa ambayo Marais watatuma wawakilishi wao ni Rwanda, Angola na Burundi.
Jumuiya 50 za Kimataifa na Kikanda zitatuma wawakilishi wao.
Aidha, Msemaji Mkuu huyo wa Serikali ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kumuaga mpendwa wao aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho katika uwanja wa Jamhuri.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.