RAIS wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweli Kaguta Museveni leo amefanya ziara ya siku moja hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo kwa pamoja wameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleane Tanga nchini Tanzani na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Aidha, kumekuwa na hali ya wananchi kutaka kuifahamu mikataba ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanzania.
Mkataba uliosainiwa leo Mei 20, 2021 Rais Samia Suluhu Hassan amesema: “Hii ni hatua muhimu kuelekea kuanza ujenzi wa bomba hilo, Tangu tuanze majadiliano yetu ya kutekeleza mradi huu, tumeshasaini mikataba muhimu mitano”.
Rais amefafanua kwamba mikataba iliyosainiwa ni Mei 2017, Tanzania na Uganda zilisaini mkataba wa ushirikiano ambao uliweka msingi wa kuanza majadiliano.
Aprili 11, 2021 nchini Uganda ilisainiwa mikataba mitatu (Mkataba mwenyeji, mkataba hodhi kati ya Uganda na kampuni ya EACOP, mkataba wa ushuru na usafirishaji na mkataba wa umiliki wa hisa ya bomba la mafuta) na leo umesainiwa Mkataba hodhi kati ya Tanzania na kampuni ya bomba la kusafirisha mafuta ya Afrika Mashariki (EACOP).
Vile vile, baada ya viongozi hao wakuu wa nchi za Afrika Mashariki walitoa tamko la pamoja kuhusu utekelezaji wa pamoja wa mradi huo wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.