Na. Josephina Kayugwa, DODOMA
KOCHA Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Masoud Juma amewataka mashabiki wa timu wawe na subira, watambue kuwa timu itafanya vizuri kwasababu timu imejipanga na imefanya mazoezi ya kutosha.
Alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi kuhusiana na mwenendo mzima wa timu, alisema moja ya ya changamoto ambayo wamekumbana nayo kama benchi la ufundi ni kuchelewa kwa mazoezi na baadhi ya wachezaji kuwa majeruhi.
“Kikosi chote kipo na kimejipanga na tunategemea ushindi katika mechi zijazo, katika kipindi cha mapumziko kupisha michezo ya Taifa Stars tumejipanga vizuri pamoja na wachezaji wote. Tunatambua mchango wa mashabiki na wadau tunaomba waendelee kuishabikia timu yao watambue kuwa Dodoma Jiji FC sio timu ya kawaida ipo makao makuu ya Nchi na ipo chini ya Taasisi wasiichukulie kawaida” alisema Masoud.
Kwa upande wake kiongozi wa wachezaji, Mbwana Hamisi alisema mechi bado zipo nyingi hivyo, mashabiki wasichoke kuwaamini na kuwaunga mkono kwasababu wanatambua jukumu lao la kuitumikia timu.
“Mashabiki tunaomba muendelee kuwa pamoja nasi tunawaahidi ushirikiano na tunawaahidi ushindi katika mechi zijazo ukizingatia mazoezi tumefanya vya kutosha” alisema Hamisi.
Alisema anawashauri wachezaji wote watekeleze majukumu yao na kutambua ni muhimu wao kama wachezaji kucheza vizuri na kupata ushindi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.