KATIBU Mkuu Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi leo Oktoba 01, 2021 wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Afrika kwa Viziwi 2021 yanayofanyika Jijini Da es salaam amewapongeza waandaaji wa madhindano ya viziwi Afrika 2021.
"Leo nchi yetu tunafarijika kuwa taifa la kwanza Afrika kuwa wenyeji wa mashindano ya warembo, watanashati na wanamitindo,... tumekuja kushuhudia vipaji ambavyo viziwi wanavyo, ni warembo, watanashati na wanaakili" amesema Dkt Abbasi.
Dkt. Abbasi amesema Afrika ilikuwa haifanyi mashindank hayo na kuwashukuru waandaji wa mashindano hayo kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji na amewahakikishia ushirikiano uliotukuka kutoka kwa Serikali.
Aidha, Dkt. Abbasi amesema Tanzania ni nchi ya amani na amewakaribisha wageni wote nchini wajisikie wapo nyumbani ikizingatiwa kupitia historia ya Harakati za Ukombozi wa zao Tanzania inamchango mkubwa katika uhuru wa nchi hizo.
Nchi za Botswana, Zimbabwe na Msumbiji ambazo zimeleta washiriki katika mashindano hayo ya mwaka huu, Tanzania ni kitovu cha historia ya ukombozi wa nchi zao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.