MWAKILISHI wa Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mhe. Sospeter Mazengo amewakambidhi washindi wa mashindano ya UMISETA ngazi ya wilaya kwa upande wa mpira wa miguu na pete. Zawadi hizo zimetolewa katika uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari Dodoma.
Zawadi hizo amezitoa kama pongezi kwa timu ya mpira wa miguu na mpira ya pete lengo likiwa ni kuwapongeza na kuwafanya waongeze juhudi zaidi katika mashindano mengine yatakayokuwa yanaendelea.
Mazengo amesema michezo ni kitu kizuri kwakuwa inaburudisha na pia michezo ni ajila, watu wengi wameweza kuajiliwa, pia michezo ni afya inafanya wachezaji wawe na afya njema, hivyo ni vyema wanafunzi wakashiriki katika michezo kwa kuwa ina faida nyingi.
‘’kwa wale mtakao chaguliwa kuunda timu ya Wilaya mtapata nafasi ya kwenda kutuwakilisha, mtambue kuwa mnajukumu la kutuwakilisha vizuri kwa kujitambua na kuonesha vipaji na kujianimi kuwa mnaweza kufanya vizuri’’, amesema Mazengo.
Pia ameweza kutoa shukurani mbalimbali kwa watu wote waliojitokeza na kutoa baadhi ya vitu mbali mbali kufanikisha mashindano haya akiwemo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde.
Kwa upande wake Afisa Elimu ya Sekondari wa Jiji la Dodoma Upendo Rweyemamu alitoa pongezi nyingi kwa washiriki pamoja na washindi kwa kuonesha ushindani na kuwa na ushirikiano katika kipindi chote cha mashindano hayo.
Rweyemamu alisema nimeandaa zawadi lengo likiwa ni kuleta ushindani na kutengeneza timu nzuri ndio maana tulitafuta wasimamizi wazuri wa michezo hiyo wasiokuwa na upendeleo wowote.
Afisa Elimu huyo alisema mashindano hayo ni mazuri kwani yanawajenga wanafunzi kiafya na kiakili hivyo anawasihi wazazi na walezi kuendelea kuwapa ushilikiano mkubwa wanafunzi hao.
‘’kutokana na hitihisho la mashindano haya hivi leo tumeweza kuunda timu yetu ambayo itakuwa na washiriki 100 tu ambao tutaanza nao kambi kuanzia tarehe 3 mwezi wa sita ili kuendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya kambi zijazo’’, alisema Rweyemamu.
Pia alisema kuwa ana imani na timu ya Wilaya iliyoundwa hivyo ushindi wote utabaki kuwa wao mpaka mwisho wa mashindano hayo kwa michezo yote ambayo watashiliki.
Aidha, Rweyemamu ametoa pongezi nyingi kwa walimu wote wa michezo wa shule zilizoshiriki katika mashindano hayo kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha kwa kipindi chote cha mashindano.
Kwa upande wake mshiriki la shindano hilo Zainabu Bakari alisema amefurahishwa na mashindano hayo kwani yameweza kumjengea uwezo mkubwa katika michezo.
‘’Mashindano haya yamenisaidia kujuana na watu wengi pamoja na kujenga uwezo wa kujiamini na kucheza mbele ya watu wengi na pia nimefurahia kwa zawadi ambayo tumepewa’’, alisema Bakali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.