OR-TAMISEMI
Mashindano ya umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yameanza rasmi Mkoani Tabora leo tarehe 17 Juni, 2024 Mjini Tabora, yakishirikisha wanamichezo mbalimbali kutoka Mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.
Mashindano ya mwaka huu ambayo yanafanyika mkoani Tabora kwa mara ya tatu mfululizo, yanatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, kutokana na uboreshwaji wa miundombinu uliofanywa na Serikali hususana kwenye eneo la viwanja.
Kwenye baadhi ya michezo iliyochezwa leo kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Tabora wavulana, Timu ya Mpira wa kikapu Wavulana ya Mkoa wa Mbeya ilianza vizuri mashindano ya mwaka huu kwa kiufunga Dodoma 51-29.
Katika mchezo mwingine Kilimanjaro ilipata ushindi wa vikapu 28 -13 dhidi ya Mkoa wa Pwani, na Kigoma ikapoteza dhidi ya Singida kwa jumla ya vikapu 48-14, na mchezo mwingine uliozikutanisha Mara na simiyu ulimalizika kwa Mara kuika na ushindi wa 23-20.
Kwa upande wa Mpira wa Wavu Wasichana, Katavi iliifunga Rukwa kwa Seti 3-0 na Manyara ikaifunga Dodoma 3-0, na kwa Wavulana Arusha ikapoteza 3-0 kwa Dar es salaam huku Mara ikiishinda Mtwara Seti 3-2
Mashindano ya UMISSETA 2024 yanayofanyika Mkoani Tabora tangu mwaka 2022, yanaandaliwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI, ikishirikiana na Wizara ya Utamaduni Sanaa na michezo, na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.
Kauli mbiu ya Mashindano ya mwaka huu inaasema “Tunajivunia mafanikio katika sekta ya elimu, michezo na Sanaa, Hima mtanzania shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.