WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako ametoa rai kwa mashirka ya Umma na Binafsi kuendeleza utaratibu wa kuwawezesha vijana wajasiliamali kufanya biashara zao kwa ufanisi ili kujenga jamii yenye usawa wa kuchochea uchumi nchini.
Ameyasema hayo wakati wa hafla ya Ushirikishwaji na Uwezeshaji vijana kiuchumi kupitia Programu ya Chipsika kiajira na Coke iliyoandaliwa na kampuni ya Coca-Cola kwanza ambayo ni Kampuni tanzu ya Coca-Cola Beverages Afrika kwa kushirikiana na Taasisi ya Ustawi wa Jamii, tarehe 29 Oktoba, Jijini Dar es salaam.
Ndalichako ametoa rai kwa wadau wengine wa maendeleo kuiga jambo hilo ambapo Kupitia program ya Chipsika Kiajira na Coke, Vijana 900 wanao jishughulisha na shughuli za upikaji wa chakula maarufu (Chips) wa Dar es Salaam wamepatiwa mafunzo ya Ujasiliamali, Uwekaji wa kumbukumbu za taarifa za biashara, Ukuzaji wa mitaji pamoja na Elimu ya saikolojia.
Aidha, Vijana hao wamekabidhiwa majiko ya gesi 300, na mitungi ya gesi yakilogramu 15 ipatayo 300, makabati ya kuweka chakula 35, Meza jumla 80 pamoja na Apron 900 zikiambatana na fulana. Vitendea kazi hivyo vinatarajiwa kuwawezesha kuongeza tija katika biashara zao.
Amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia imendeleea kuweka Sera, Mipango na programu wezeshi za kuwainua Vijana nchini ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao hadi sasa tayari umewezesha kutoa mikopo ya Shilingi bilioni 8.13 kwa zaidi ya vijana 1,057.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Coca-Cola Kwanza, Unguu Sulay, amebainisha kuwa kanuni hiyo imekuja na mpango huo kabambe wenye lengo la kwenda kutambua juhudi zifanywazo na vijana nchini ili kuwajengea uwezo vijana wajasiliamali wa chakula ili kuweza kuongeza ufanisi wa shughuli zao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.