Na. Elizabeth S. Dai
Habari- DODOMA RS
Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) yamekua yakichagiza jitihada za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Mhe. Dorothy Gwajima ambae amemuwakilisha Mgeni rasmi Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango katika Kongamano la mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali lililohitimishwa leo Agosti 13, 2025 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma.
“Ni ukweli usiopingika kuwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali yamekua yakichagiza jitihada za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia utekelezaji wa miradi hususani katika sekta ya afya, kilimo, elimu, maji , mazingira, utawala bora, maendeleo ya jamii, miundombinu, mifugo na uvuvi pamoja na sekta nyingine.”
Akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatekeleza majukumu mbalimbali katika kupambana na changamoto za kiuchumi na kijamii kwa lengo la kujenga Taifa bora kwa kuzingatia upatikanaji wa huduma muhimu kwa makundi yote.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Bw. Jasper Makalla amesisitiza ushirikiano kati ya Mashirika ya Kiserikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Sekta Binafsi katika kuleta maendeleo katika jamii.
Kongamano hilo lililobeba kaulimbiu inayosema “Tathmini ya Miaka Mitano ya Mchango wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa: Mafanikio, Changamoto, Fursa na Matarajio” limeambatana na uzinduzi wa kitabu cha muongozo pamoja na kamati ya Taifa yenye wajumbe kutoka taasisi mbalimbali ambayo itasimamia kazi zote za Mashirika hayo kwa ushirikiano.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.