Na. Dennis Gondwe, DODOMA
SHULE ya sekondari Dodoma imekuwa ikifundisha masomo ya ziada yakilenga kuwaandaa wanafunzi kujiajiri wanapomaliza shule ili waweze kutoa mchango katika maendeleo ya taifa lao.
Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mkuu (utawala) wa Shule ya Sekondari Dodoma, Mwl. Euphrasia Kiowi alipokuwa akiongelea umuhimu wa masomo ya ziada katika kuwaandaa wanafunzi baada ya kuhitimu masomo yao.
Mwl. Kiowi alisema kuwa shule yake pamoja na kufundisha masomo ya kawaida kama zilivyo shule nyingine inafundisha na masomo ya ziada. “Masomo ya ziada yanayofundishwa shuleni hapa ni ‘food and nutrition’, ICT, michezo, uchoraji na sanaa, lugha ya kichina na kifaransa. Masomo haya ya ziada tunaamini yanamuandaa zaidi mwanafunzi kuweza kujiajiri na kujitegemea anapomaliza shule. Mfano Somo la uchoraji na sanaa linamuwezesha mwanafunzi kutengeneza mabango ambayo kwa siku hizi yanashika kasi sana katika kufikisha ujumbe. Hivyo, kumsaidia mwanafunzi kujiajiri. Michezo itawawezesha vijana kujiajiri kupitia michezo” alisema Mwl. Kiowi.
Lugha ya kichina na kifaransa ni muhimu kwa mawasiliano, alisema. “Tunafahamu kuwa lugha ya kichina na kifaransa zinakuja juu sana kipindi hiki, hivyo kumfundisha mwanafunzi lugha hizo ni kumsaidia kwenye mawasiliano yatakayomuwezesha kufanya shughuli mbalimbali na watu wa mataifa hayo” alisema Mwl. Kiowi.
Shule ya sekondari Dodoma kwa kidato cha V-VI ina tahasusi za PCM, PCB, PMC, CBG, EGM, HGK na HGL ikiwa na jumla ya wanafunzi 1,539 kati yao wasichana ni 984 na wavulana ni 545.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.