SERIKALI imeazimia kuendelea katika matumizi ya Mifumo ya utoaji na usimamizi wa huduma ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma stahiki katika maeneo ya vijijini na mijini kupitia vituo mbalimbali vya huduma za kijamii, kiuchumi na kiutawala.
Hayo yamebainishwa leo Julai 10, 2024 wakati wa Mkutano wa ufunguzi wa kikao kazi cha Upangaji wa pamoja wa Mradi wa Usimamizi na Uimarishaji wa Mifumo Sekta ya Umma (PS3+) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, jengo la Mkapa Jijini Dodoma.
Kikao kazi hicho kilichoongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt. Charles Msonde kimeangazia ushirikishwaji wa wananchi katika matumizi ya mfumo kwa ajili ya maendeleo endelevu.
“Mfumo wa Uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha katika ngazi ya shule za sekondari na msingi, vituo vya kutolea huduma za afya, ofisi za Kata, Vijiji na Mitaa ambapo umeleta uwazi, uwajibikaji na kudhibiti matumizi ya fedha katika ngazi za msingi za Mamlaka za Serikali za mitaa” Amesema Dkt. Msonde
Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya, ametoa rai kwa Watumishi wote kuiweka Programu hii katika mikono yao na kuichukilia kwa uzito ambao utaongeza ufanisi juu ya ushiriki wa wananchi katika kuibua na kupokea miradi ya Maendeleo inayoletwa na Serikali.
Kadhalika, Mkuu wa Timu ya Uboreshaji Mifumo kutoka Shirika la USAID Tanzania Bw. Godfrey Nyombi, amesema kuwa Mifumo hii inatumika kwa shughuli za kila siku kama vile usimamizi wa fedha, Mipango, taarifa, mawasiliano kwa wananchi na inasomana na mifumo mingine hivyo kurahisisha shughuli za kimaendeleo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.