HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inafanya juhudi za makusudi kuhakikisha vyanzo vyake vyote vya mapato ya ndani vinaendelea kukusanywa kwa kutumia Mashine za Kielektroniki za Kukusanyia Mapato (Point-of-sell Machine POS).
Hayo yamesemwa leo (tarehe 13 Novemba, 2021) na mmoja wa maafisa TEHAMA wa Jiji la Dodoma, Neema Njau (pichani kushoto) alipokuwa akiongea na tovuti hii ofisini kwake. Tovuti hii ilimkuta Njau akitekeleza majukumu yake kwa kutoa elimu ya matumizi bora na sahihi ya POS kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Miganga Angela Kullaya kutoka kata ya Mkonze. Lengo ni kuwawezesha watumishi wa Jiji kuendelea kukusanya mapato ya Halmashauri kwa ufanisi tukitumia mfumo na vifaa vya kielektroniki kukusanya mapato.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Miganga kutoka kata ya Mkonze alisema amefurahia maelekezo ya namna ya kutumia kifaa cha kielektroniki cha kukusanyia mapato - POS na ameelewa vizuri. "Nashukuru nimeelewa vizuri maelekezo ya kifaa hiki, na nimeanza mwenyewe kuchangia Mtaa wangu kwa kuchanga shilingi elfu tano kama mchango wa jamii kwa maendeleo ya mtaa wetu" alisema Mwenyekiti huyo kwa furaha.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.