• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mavunde agawa vifaa vya kujikinga na Corona

Imewekwa tarehe: June 1st, 2020

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amekabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona kwa shule zote zenye kidato cha tano na sita katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Msaada huyo ameukabidhi leo kwa Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Upendo Rweyemamu kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viunga vya Halmashauri hiyo.

Mavunde amesema kuwa vifaa alivyotoa vinalenga kuwahakikishia wanafunzi wa kidato cha sita wanakuwa salama katika kipindi chote watakachokuwa shuleni. “Leo nipo hapa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kutoa msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa covid-19 kwa shule zote za serikali na binafsi katika Jimbo la Dodoma Mjini. Ombi langu kwa wanafunzi katika Jimbo la Dodoma Mjini ni kuendelea kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona. Viongozi tutahakikisha wanafunzi wote wa kidato cha sita wanafanya mitihani kwa usalama mkubwa” alimalilzia Mavunde.

Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia kazi, ajira, vijana na watu wenye ulemavu aliwatakia heri wanafunzi wa kidato cha sita katika mitihani yao. Alimuomba Mungu kuwawezesha wanafunzi hao kufanya vizuri na kufaulu vizuri mitihani yao.

Aidha, alimshukuru Rais wa Tanzania kwa uamuzi wake makini kuruhusu shule za kidato cha sita kufunguliwa. “Napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli kwa uamuzi wake makini na madhubuti kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha sita wanarejea shuleni kuanzia leo tarehe 1 mwezi Juni kujiandaa na mitihani yao ya kidato cha sita” amesisitiza Mhe. Mavunde.

Vilevile, aliwashukuru wakuu wa idara ya Elimu Msingi na Sekondari kwa ushirikiano mzuri wanaompatia kutekeleza majukumu yake. “Ninajivunia sana wakuu hawa wa idara kwa kazi nzuri wanayofanya katika Jiji la Dodoma. Nawashukuru pia wakuu wa shule na waratibu elimu kata kwa kazi nzuri wanayofanya” aliongeza Mavunde.

Kwa upande wake, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwalimu Upendo Rweyemamu alisema kuwa mbunge huyo anafanya kazi kubwa kukuza sekta ya elimu. Napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini kwa kazi kubwa, amekuwa mstari wa mbele sana katika kukuza elimu. Mbunge huyu ni mpambanaji sana hivyo, ameona atoe vifaa vya kupambana na virusi vya corona katika shule zote 11 zilizopo katika Halmashauri ya Jiji ili wanafunzi wetu wawe salama.

Nae mkuu wa shule ya sekondari ya Maria De Mattias, Mwalimu Lowaeli Lyimo akiongea kwa niaba ya wakuu wa shule, alimshukuru Mbunge huyo kwa kuwa bega kwa bega na shule za serikali na binafsi katika halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Mbunge huyu amekuwa karibu sana na shule kwa kuzitembelea na kuongea na wanafunzi na kuwatia moyo katika masomo yao. Tunamshukuru sana kwa kutoa msaada huu kwa shule za jiji la Dodoma” alisema Mwalimu Lyimo. Vilevile, aliwashukuru maafisa elimu wa Halmashauri kwa ushirikiano wanaoutoa kwa shule hizo na kuitaka jamii kuendelea kuwaombea wanafunzi hao waweze kufanya mitihani yao na kufaulu vizuri.

Vifaa vya kujikinga na virusi vya corona vilivyokabidhiwa ni majaba makubwa ya kuhifadhi 160, ndoo 44, sabuni ya maji zaidi ya lita 300 na sabuni za kawaida na vitakasa mikono vyote vikiwa na gharama ya shilingi milioni mbili.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (kulia) akimkabidhi vitakasamikono Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Maria De Mattias, mwlimu Lowaeri Lyimo (kushoto). katikati ni Afisa Elimu Msingi Jiji la Dodoma, Mwalimu Joseph Mabeyo akishuhudia tukio hilo

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (kulia) akiongea na Waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya kujikinga na virusi vya corona kwa shule zenye kidato cha tano na sita jijini Dodoma. Kushoto ni Afisa Elimu Msingi Jiji la Dodoma, Mwalimu Joseph Mabeyo.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde (katikati) akifurahia jambo na Afisa Elimu Sekondari Jiji la Dodoma, Mwalimu Upendo Rweyemamu (kulia), Kushoto ni Afisa Elimu Msingi Mwalimu Joseph Mabeyo. 



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.