Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amekabidhi sare za michezo 120 kwa timu ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) inayojiandaa na mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa wa Dodoma ili kuchochea hamasa kwa wanamichezo.
Sare hizo zilikabidhiwa kwa timu ya UMISSETA ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Sylas Sylivester katika hafla iliyofanyika shule ya sekondari Dodoma.
Sylivester alisema “mnamfahamu mbunge wenu ni mtu wa michezo, ameniagiza miwaletee vifaa vya michezo kulingana na idadi yenu. Nimewaletea ‘tracksuits’ 120. Sisi ni watoto wa mjini. Tuhakikishe tunachukua makombe yote, na ninaamini sura hizi zitatuletea ushindi. Mbunge wenu anawasalimia”.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Upendo Rweyemamu alimshukuru mbunge kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wanafunzi hao. “Labda niwaambie wanangu mimi nimefanya kazi halmashauri nyingi, lakini ushirikiano nilioupata hapa kutoka kwa Mbunge sijawahi kuupata mahali pengine. Tangu nimefika hapa amekuwa akidhamini “tracksuits” hizi kila mwaka. Umwambie sisi tunamshukuru sana na hatutamuangusha tutahakikisha tunatafuta ushindi kwa ajili yake” alisema Rwenyemamu.
Nae mwanafunzi wa shule ya sekondari Bihawana, Bukuyu Bukuyu alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini kwa kuwaletea vifaa vya michezo na kuahidi ushindi. “Napenda kutanguliza shukrani zangu kwa mheshimiwa mbunge kwa kutuletea vifaa vya michezo hivyo tunaahidi makombe yote yatabaki mjini kulingana na walimu wetu walivyotufundisha. Tunamuomba mbunge wetu aendelee kuwa pamoja na sisi” alisema Bukuyu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.