Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde leo ametekeleza ahadi yake ya kuezeka soko la Wafanyabiashara wa Mboga mboga na Matunda wa Soko la Bonanza-Chamwino Jijini Dodoma kwa kukabidhi kwa Uongozi wa soko jumla ya mabati 400 na mabomba 100 vyote vikiwa na thamani ya Tsh 25,000,000 ili kuanza ujenzi katika soko hilo.
Mbunge Mavunde amekabidhi leo vifaa hivyo ambavyo ujenzi wake ukikamilika utasaidia sana kupunguza adha ya jua na mvua ambalo limekuwa likiwakabili wafanyabiashara hao wadogo kwa muda mrefu.
"Kwa kuwa Rais Magufuli ametupa heshima ya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi,ni wajibu sasa sisi kama viongozi kuutafsiri uamuzi huu kwa vitendo kwa kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo miundombinu ya masoko ili iendane na hadhi ya Jiji La Dodoma kwa hivi sasa.
Wafanyabiashara wadogo wa matunda na mboga mboga sasa mtapata nafasi ya kufanya biashara zenu katika mazingira ambayo ni rafiki tofauti na awali ambapo mlikuwa kwenye jua kali na mvua." alisema Mavunde.
Viongozi wa Soko la Bonanza, CCM Kata na Diwani aliyemaliza muda wake wa kisheria Mhe. Jumanne Ngede wote kwa pamoja wamemshukuru Mbunge Mavunde na Ndugu Grayson Mwakasege - Meneja wa Kampuni ya mabati ya ALAF kwa kufanikisha upatikanaji wa vifaa hivyo na kuahidi kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Picha mbalimbali za matukio:
Mheshimiwa Anthony Mavunde akiongea na wafanyabiashara wa soko la Bonanza - Chamwino Jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.