MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini Wakili Msekeni Ally Mkufya leo tarehe 29 Oktoba, 2020 majira ya saa 12:00 jioni amemtangaza mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anthony Peter Mavunde kuwa mshindi wa kinyang'anyiro cha Ubunge wa Jimbo la Dodoma mjini.
Akitangaza matokeo hayo hadharani mbele ya waandishi wa habari na wananchi wa Dodoma nje ya ofisi yake leo, Wakili Mkufya amesema Mavunde amepata kura 86,656 sawa na asilimia 86.44 ya kura halali zilizohesabiwa akimshinda mpinzani wake kutoka Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Aisha Madoga aliyepata kura 13,589 sawa na asilimia 13.56 ya kura halali zilizopigwa.
Aidha, Wakiri Mkufya amesema katika uchaguzi huo, Wapiga kura walioandikishwa katika Jimbo lake ni watu 335,324 ambapo idadi halisi ya waliopiga kura ni watu 102,769, kura halali zilikuwa 100,245 na kura zilizokatialiwa ni 2,524.
Kwa matokeo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini Wakili MMsekeni Ally Mkufya amemtangaza Anthony Peter Mavunde kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge na kumkabidhi cheti cha ushindi.
Baada ya kukabidhiwa cheti cha upshindi mbunge huyo mteule alitoa shukurani zake za dhati kwa wanadodoma kwa kumuwezesha kupata ushindi huo mkubwa wa zaidi ya asilimia 86.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.