WALIMA Zabibu kutoka Makao Makuu ya Nchi Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana wakiwa ugenini dhidi ya Mbeya Kwanza ya Mbeya.
Mchezo huo ulichezwa Leo tarehe 17/10/2021 katika Dimba la Sokoine huku ukitawaliwa na nguvu na ubabe wa hali ya juu na timu zote hazikufanikiwa kuziona nyavu za mwingine licha ya Dodoma Jiji kupata nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia.
Akizungumza baada ya mchezo huo Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji Mbwana Makata amesema kuwa ulikua mchezo wa aina yake na kukiri kuwa walikua na nafasi kubwa ya kushinda lakini umakini mdogo wa wamaliziaji wake ukawafanya washindwe kuondoka na alama 3 wakiwa ugenini.
Makata amesema kuwa mchezo huo umeshamalizika na wanatupia macho kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Tanzania Prisons ambao utachezwa nyumbani katika uwanja wa Jamhuri Dodoma tarehe 24/10/2021.
"Vijana wangu wamepambana nawapongeza lakini kama washambiliaji wetu wangeongeza umakini tungepata alama tatu" alisema Makata.
Katika mchezo huo mlinzi wa Dodoma Jiji Agustino Nsata aliumizwa kwa kupigwa kiwiko na kutolewa nje kwaajili ya matibabu huku Kocha msaidizi wa timu hiyo Renatus Shija alipewa kadi nyekundu na kutolewa nje na.kuzua sintofahamu kwa benchi la ufundi la timu ya Dodoma Jiji.
Matajiri hao wa Zabibu wamesalia katika nafasi nane kwenye msimamo wa 'NBC Premier League', wakiwa na alama nne huku wakicheza michezo mitatu ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.