• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mbogamboga na Matunda kupata soko katika nchi za Ulaya

Imewekwa tarehe: February 28th, 2020

Makampuni kumi na tano (15) yaliyojumuisha wazalishaji pamoja na wasafirishaji wa bidhaa za mbogamboga na matunda wajiongezea fursa katika soko la Ulaya kufuatia ushiriki wao katika Maonesho ya Kimataifa ya Mbogamboga na Matunda yajulikanayo kama Fruit Logistica 2020 yaliyofanyika tarehe 5 hadi 7 Februari, 2020 mjini Berlin nchini Ujerumani.

Mazao yaliyovutia wanunuzi na wadau wengine katika maonesho hayo ni pamoja na parachichi, rasiberi, pasheni, ndimu zisizo na mbegu, njegere, snow pears na sugar snaps, maharage machanga (green beans), french beans, babycarrots, aina mbalimbali za jamii ya pilipili, viungo vya chakula kama vile tangawizi, nana (mint), kitunguu jani (chives), tikiti maji na mafuta ya parachichi.

Taarifa iliyotolewa nchini na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mheshimiwa Balozi Abdallah S. Possi imeeleza kuwa mafanikio ya ushiriki wa Tanzania yamekuwa makubwa kutokana na makubaliano ya kimkakati yaliyofikiwa baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na wanunuzi wa mbogamboga na matunda wa nchi za Ulaya, hali inayoleta viashiria chanya vya kupata masoko makubwa. Makubaliano hayo yanatarajiwa kuimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi za Ulaya na hivyo kuvutia uwekezaji katika sekta husika nchini.

Wafanyabiashara wameweza kukutana na kuingia makubaliano na wanunuzi, wabia wa biashara na wadau muhimu kama vile Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) na Taasisi ya Kimataifa ya GLOBALG.A.P inayoshughulikia viwango vya ubora w bidhaa za kilimo na mifugo. Taasisi hizo ni wadau muhimu katika kuwawezesha wazalishaji kutumia njia salama, sahihi na endelevu katika uzalishaji na kuwaunganisha na masoko ya kikanda na kimataifa. Vilevile washiriki waliweza kujifunza teknolojia za kuzalisha, kusindika, kufungasha, kuhifadhi na kusafirisha mazao ya kilimo ili kukidhi mahitaji ya soko la Ulaya.

"Binafsi nilikutana na mzalishaji kutoka Tanzania ambaye ameingia makubaliano na muwekezaji kutoka Ujerumani. Hii inamaanisha maonesho haya pia yalikuwa ni fursa kwa wazalishaji wa Tanzania kutafuta wabia wa biashara" amesema Mhe. Balozi Possi.

Aliendelea kusema kuwa, mkakati wa ubalozi ni kuandaa na kuratibu matukio maalum kama vile Maonesho, Semina, Mikutano ya ana kwa ana ya wafanyabiashara ili kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wadau muhimu wa nchi za Ulaya. Vilevile, Ubalozi wa Tanzania uliopo Berlin umekuwa ukihimiza ushiriki wa Tanzania katika maonesho yanayofanyika nchini humo ili kutafuta fursa zaidi za kibiashara.

Mhe. Balozi ameshauri wazalishaji kuimarisha umoja miongoni mwao ili wapate urahisi wa kuwa na wingi wa bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora vinavyohitajika katika soko kubwa la Ulaya kwa ujumla wake.

Fruit Logistica ni Maonesho makubwa ya matunda na mbogamboga katika Bara la Ulaya ambayo kwa mwaka huu yamevutia ushiriki wa waoneshaji zaidi ya 3,300 kutoka kila hatua ya mnyororo wa ugavi (supply chain) ambao walitoka katika nchi 93 duniani. Kadhalika,  maonesho yalivutia watembeleaji zaidi ya 78,000 kutoka nchi zaidi ya 135.

Kwa Tanzania, TanTrade kwa kushirikiana na Kituo cha Biashara ya Kimataifa (ITC) na Taasisi inayosimamia wadau wa matunda na mbogamboga, maua, viungo vya chakula na bidhaa zake (TAHA) iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye maonesho hayo ikiwa ni matokeo ya mafanikio ya utekelezaji wa mradi wa Market Access Upgrade Programme (MARKUP) wenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa masoko ili kuongeza mauzo ya nje ya nchi kwa bidhaa za kilimo.

  • Tovuti hii iliwahi ku-ripoti juu ya maonesho ya Fruit Logistica 2020

Chanzo:Taarifa kwa Umma - TanTrade

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.