NAIBU WAZIRI wa Kilimo Mh. Anthony Mavunde amewahakikishia wakulima nchini juu ya upatikanaji wa mbolea ya ruzuku kwa wakati katika msimu wa kilimo unaokuja ili kutatua changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita.
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo jana katika viwanja vya Mwembetogwa,Manispaa ya Iringa wakati akipokea maelekezo ya Katibu Mkuu wa CCM Cde. Daniel Chongolo aliyetaka wananchi kusikia kauli ya serikali juu ya upatikanaji wa mbolea kwa wakati kwa msimu wa kilimo unaokuja.
“Ndugu Katibu Mkuu kwanza tunaishukuru serikali ya CCM chini ya uongozi wa Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuja na mpango wa mbolea ya ruzuku kwa lengo la kumpunguzia mkulima gharama za bei juu ya pembejeo.
Katika Msimu ujao wa Kilimo tutahakikisha mbolea inawafikia mapema wakulima wakiwa wametoka tu kuuza mazao yao,tumeiongezea pia mtaji wa Shilingi Bilioni 40 Kampuni ya Mbolea (TFC) ili iweze kununua na kusambaza mbolea nchi nzima, pia tutaongeza vituo vya mauzo maeneo ya karibu na wakulima sambamba kutumia AMCOS kama wakala wa mbolea katika baadhi ya maeneo.
Pia tumetoa maelekezo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) kuhakikisha wanakaa na wazalishaji wa ndani na waingizaji ili
kuanza kufungasha mbolea katika ujazo wa kilo 5,15,25 na 50 ili wakulima wanunue kutokana na mahitaji yao” Alisema Mavunde.
Naye Katibu Mkuu wa CCM Cde. Daniel Chongolo ameiagiza wizara ya Kilimo kuhakikisha inarekebisha haraka miundombinu ya umwagiliaji katika eneo la Ruaha Mbuyuni na kutumia fursa hiyo palia kuwataka watumishi wote wa serikali kuwatembelea wananchi na kusikiliza kero zao msingi na kutoa majawabu ya changamoto zao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.