Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mh Anthony Mavunde amewaagiza Viongozi wa Kata ya Chahwa kufanikisha upatikanaji wa ramani na vibali vyote muhimu vya Ujenzi ili kuanza Ujenzi wa Shule ya Sekondari katika eneo la Mahoma Makulu.
Mbunge Mavunde ameyasema hayo jana katika Mtaa wa Mahoma Makulu,Kata ya Chahwa wakati wa mkutano wa hadhara wa kutambulisha Viongozi wapya wa Serikali za Mitaa waliopatikana wakati wa Uchaguzi Novemba,2019.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake Mzee Paschal Ngh'angala amemuomba Mbunge Mavunde kutatua changamoto ya ukosefu wa Shule ya Sekondari inayowalazimu watoto kutembea umbali mrefu kwenda kupata elimu kwenye Shule za kata ya jirani ilihali wao wana eneo la ukubwa wa ekari 8 lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari.
Akijibu kero hiyo, Mbunge Mavunde amewataka wananchi hao kwa kushirikiana nae kwa pamoja waanze ujenzi huo na kwamba Serikali itawakuta njiani huko baadaye ili kabla ya Mwezi April taratibu za Ujenzi ziwe zimeanza ambapo atatoa matofali 1000 na mifuko ya saruji 50 katika hatua ya awali na kusimamia ukamilishwaji wake kama ambavyo amefanya katika Shule zingine alizojenga na baadhi ambazo anaendelea kujenga katika Jijinla Dodoma.
Akitoa maelezo ya awali Diwani wa Kata ya Chahwa Mh Sospter Mazengo amemueleza Mbunge Mavunde kwamba atasimamia taratibu zote za awali za Ujenzi wa Shule hiyo ya Sekondari ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa Vibali vya Ujenzi na ramani ya michoro ya majengo mpaka kukamilika kwake na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika kushiriki moja kwa moja katika ujenzi wa shule hiyo.
Picha za matukio mbalimbali:
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.