Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde kwa kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM hasa katika Sekta ya Elimu kutokana na mchango mkubwa anaoutoa katika kuboresha miundombinu ya majengo ya shule na matundu ya vyoo katika Jimbo la Dodoma Mjini.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge wakati wa uzinduzi wa darasa lililojengwa kwa ufadhili wa Mbunge Mavunde kutokana na maombi ya Wananchi hao mwaka 2015 wakati wa Kampeni ya Uchaguzi ambapo kero kubwa iliyosemwa na wananchi ilikuwa ni upungufu wa madarasa katika Shule ya Msingi Chang'ombe B na Mbunge Mavunde kuahidi kuitatua pindi atakapochaguliwa.
"Wakati nakuja Dodoma nilikukuta una zoezi la kugawa matofali 32,000 na mifuko ya Saruji 3,200 kwa Kata zote 41 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo, leo tena umeniita kwa jambo hili kubwa la kufungua Darasa. Unawatendea haki sana wananchi wako na Mungu akuongoze uendelee kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya Elimu" Alisema Dkt. Mahenge.
Akitoa salamu zake, Mbunge Mavunde ameeleza kwamba alianza utekelezaji wa ahadi yake hiyo mwaka 2016 kwa kuanza ujenzi huo polepole na kukamilika rasmi September, 2019 kwa gharama ya Tsh 15m (milioni kumi na tano) na hivyo kutatua changamoto hiyo ya upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo awali wanafunzi walikuwa wanapata changamoto ya mazingira wezeshi ya kusomea.
Pamoja na darasa hilo, Mbunge Mavunde amekabidhi madawati 30 kwa ajili ya darasa hilo na pia ameanza ujenzi wa Ofisi ya walimu shuleni hapo huku akilipongeza Jiji La Dodoma kwa kutenga kiasi cha Shilingi Bilioni nane kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na miundombinu mbalimbali kwa Shule za Msingi na Sekondar Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (mwenye skafu shingoni), Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde (wa pili kushoto mbele) na Diwani wa kata ya Chang'ombe Mhe. Bakari Fundikira wakiongoza wananchi wa kata ya Chang'ombe, waalimu na wanafunzi kwenda kuzindua darasa lililojengwa kwa ufadhili wa Mbunge Mavunde.
Madarasa 30 (thelathini) yaliyotolewa na Mbunge Anthony Mavunde kutumika katika darasa aliloliljenga kutimiza ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 alipokuwa akijibu moja ya kero zilizokuwa zikiwasumbua wananchi wa kata ya Chang'ombe jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge akimpongeza Mbunge Anthony Mavunde kwa kasi kubwa ya kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kuhusu uimarishaji wa Miundombinu ya Elimu.
Mbunge Anthony Mavunde (katikati) akifurahia pamoja na wanufaika wa darasa alilolijenga (wanafunzi) kwa ajili ya shule ya msingi Chang'ombe B.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.