MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde leo ametembelea Shule ya Sekondari Chihanga kuangalia maendeleo ya shule pamoja na kuwasalimia na kuwatakia kheri wanafunzi wa kidato cha IV walioweka kambi shuleni hapo kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya kidato cha IV ya kitaifa itakayofanyika Novemba, 2021.
Mhe. Mavunde amewataka wanafunzi waongeze juhudi katika masomo yao ili kupata maarifa ya kusaidia kuliletea maendeleo Taifa la Tanzania sambamba na kuwatakia kheri wanafunzi wa kidato cha IV katika mitihani yao na kuwataka kuongeza juhudi zaidi kwa kipindi hiki kifupi kilichobakia kabla ya mitihani hiyo.
Akiwa shuleni hapo, Mhe. Mavunde amekabidhi seti moja ya Kompyuta na 'Printa' kwa ajili ya kuchapisha mitihani ya wiki na hivyo kuwapunguzia mzigo wazazi wa wanafunzi hao ambao walikuwa wanachangia kila wiki kwa ajili ya kuchapisha mitihani katika maduka binafsi ya vifaa vya ofisi na shule.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi, Diwani wa Kata ya Chihanga Mhe. Alice Kitendya amemshukuru Mbunge Mhe. Mavunde kwa jitihada kubwa anazofanya kwenye sekta ya elimu na pia kwa kusikia kilio cha wazazi hao ambao walipeleka ombi rasmi la kusaidiwa kompyuta na 'printa' kwenye ofisi ya Mbunge.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.