MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde amwapongeza wanachama wa kikundi cha vijana cha IJEN waliopo Dodoma kwa matumizi sahihi ya teknolojia katika kuleta ufumbuzi wa changamoto katika jamii.
Mheshimiwa Mavunde ametoa pongezi hizo wakati akifungua duka la bidhaa za mboga mboga la kikundi cha IJEN almaarufu kama ‘Soko la Kiganjani’ lililopo Capital City Mall ambapo mteja anaweza kuagizidhaa zake akiwa nyumbani kupitia simu na bidhaa zikamfikia mahali alipo bila yeye mwenyewe kwenda dukani.
“Nawapongeza sana vijana wote mliokuja na wazo hili la kibunifu na kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za nyumbani kwa kutumia teknolojia ya simu, jambo ambalo litampunguzia muda na usumbufu mteja.
Najua hiki ni kikundi na mna ndoto nyingi na nigependa kuwaona mnafikia malengo yenu, binafsi nitawasaidia kuwalipia gharama zote za kusajili Kampuni ili muwe katika mfumo wa kibiashara kwa kampuni sambamba na kuwatafutia fursa za kuongeza mtaji wenu wa kibiashara” alisema Mhe. Mavunde.
Naye Mwenyekiti wa kikundi hicho, John Ngalaba akiongea kwa niaba ya wanakikundi amemshukuru Mbunge Mhe. Mavunde kwa kukubali kuwaunga mkono katika adhma yao ya utoaji wa huduma za bidhaa za nyumbani kwa wananchi wa Jiji la Dodoma na kuahidi kuboresha huduma zaidi ili kuwafikia wananchi wengi kwa kutumia teknolojia ya simu.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua rasmi 'Soko Kiganjani' uzinduzi uliofanyika eneo la Capital City Mall Jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.