Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WANANCHI wametaarifiwa kuwa mchakato wa kugawa maeneo ya mitaa ambayo yanaonekana makubwa ili kusogeza huduma karibu na wananchi unaanzia katika ngazi ya mtaa.
Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Diwani wa Kata ya Iyumbu, Richard Sutuchi aliyetaka kujua utaratibu wa wa kugawa maeneo ya mitaa ili kusogeza huduma kwa wananchi katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Fungo, alisema kuwa utaratibu wa kugawa mitaa unaanzia katika mitaa husika. “Mapendekezo yanatoka katika mitaa husika na utaratibu huo unapelekwa katika kikao cha kamati ya maendeleo ya kata hadi halmashauri. Hivyo, mchakato uanzie kwenye mtaa” alisema Fungo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.