Wito umetolewa kuzingatia maelekezo yatakayotolewa na Tume ya uchaguzi ili Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata waweze kutekeleza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Adam Mkina alipokuwa akifungua mafunzo ya uandikishaji kwa Maafisa Waandikishaji Wasaidizi wa ngazi ya Kata katika Jiji la Dodoma. Mafunzo haya yanafanyika kwa siku 2 katika Ukumbi wa Shule ya St. Peters Clever eneo la Ihumwa jijini Dodoma.
Mkurugenzi msaidizi huyo amewapongeza washiriki wote walioteuliwa na Tume kuendesha na kusimamia zoezi hilo muhimu la Uandikishaji wa Wapiga Kura. Amesema uteuzi huo umetokana na ujuzi na taaluma walizonazo katika utekelezaji wa majukumu ya kitaifa.
Madhumuni ya mafunzo ni juu ya wajibu na taratibu za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Mafunzo haya pia yanalenga kuwawezesha wanasemina kupata uelewa ujazaji wa fomu zote zitakazotumiaka kwenye zoezi pamoja na jinsi ya kutumia kwa ufasaha BVR Kit.
Aidha aliwaasa washiriki kuhakikisha kuwa wanatunza vifaa vyote vitakavyotumika katika zoezi la uboreshaji wa daftari kwani vifaa hivyo vimenunuliwa kwa gharama kubwa. Amewakumbusha kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanyika kwa ufanisi mkubwa.
Mkina ametoa rai kwa wanasemina kuwa na ushirikiano mkubwa kati yao, Serikali, Vyama vya siasa na Wadau wengine wote na endapo watakuwa na hitaji lolote wasisite kuwasiliana na Tume ili kuona changamoto zote zitakazojitokeza wakati wa zoezi zinatatuliwa.
Mwishoni aliwatakia mafunzo memo na utendaji mzuri katika zoezi zima la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura. Semina hii inajumuisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi 41 kutoka kata zote za Halmashauri ya Jiji la Dodoma, na itaendeshwa na wawezeshaji kutoka ngazi ya Halmashari pamoja na maafisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.