WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amekemea utendaji usioridhisha wa watumishi wa afya katika maeneo ya kutolea huduma nchini kwa kuwa unaenda kinyume na maadili ya utumishi.
Maelekezo ya Mchengerwa yametolewa kwa niaba na Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume alipotembelea kituo cha Afya Mji Mwema Manispaa ya Songea ambacho hivi karibuni taarifa zilisambaa mtandaoni zikionesha wahudumu wa Afya kutowajibika kumsaidia mama mjamzito.
“Tunatoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kuwa tusingependa kusikia mteja anacheleweshewa huduma kwasababu za kwetu binafsi ambazo ni kinyume na miongozo ya kitaaluma na tunakoelekea leseni lazima itashikiliwa” amesema
Akisisitiza maelekezo ya Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema “kituo chochote (afya) ndani ya halmashauri yoyote ambayo itasababisha ‘either’ ulemavu kwa mteja awe mjamzito,mtoto au kusababisha kifo na ukifanyika uchunguzi ikabainika kwamba kilichosababisha ni uzembe hatua zitakwenda kwa muhusika,mganga mfawidhi,mganga mkuu wa Halmashauri na mganga mkuu wa mkoa” amesema Dkt. Mfaume
Akizungumzia hatua zilizochukuliwa na Halmashauri kwa uzembe wa watoa huduma uliojitokeza katika kituo cha Afya Mji Mwema, mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Bashiru Mhoja amesema watumishi waliohusika wamewajibishwa huku akiwasihi watumishi wengine kutoshusha morali ya kutoa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Dkt. Alice Kitindi, Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Mji Mwema ameahidi kusimamia ipasavyo utoaji wa huduma katika kituo hicho na kuahidi kutojirudia kwa matukio ya utovu wa nidhamu katika kituo hicho.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.