MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amefurahia ushirikiano wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana na Idara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi kwa katika kuviunganisha vikundi vya wajasiliamali na kuvisaidia kukua kiuchumi.
Prof. Mwamfupe alisema kuwa ushirikiano wa idara hizo ni chachu kwa maendeleo. “Tunachokiona hapa ni ubunifu wa hali ya juu ya wataalam wetu. Katika hili tukio tunajifunza jambo moja kubwa kwamba hawa wataalam tukiwaamini, watajiamini. Nimekuwa nipenda ifeke hatua Jiji la Dodoma tunaboresha ufugaji wa watu wanaozunguka maeneo ya mji. Maeneo yao tumeyachukua kwa ajili ya maendeleo ya mji. Wananchi hao watafuga wapi kama wanamazoea ya ufugaji wa Ng’ombe wa kawaida wanaochukua maeneo makubwa” alihoji Mshahiki Meya.
Mstahiki Meya huyo alisema kuwa mpango wa halmashauri ni kugawa ngombe 150 kwa kipindi cha miezi 12 ijayo. Aidha, aliwataka vijana kuwa tayari kujikita katika sekta ya mifugo. “Vijana kaeni siyo mkao wa kula, najua mmeshana, njooni mle, tunafedha za kutosha, acha kufuga kwa ‘WhatsApp’ njoo jifunze, njoo ufuge. Kuna vijana wamemaliza vyuo njoo mfuge” alisisitiza Prof. Mwamfupe.
Akiongelea upatikanaji wa Ng’ombe hao, Nabalang’anya alisema kuwa Idara yake kwa kushirikiana na Idara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi walihakikisha kuwa fedha zinazoingizwa katika akaunti za vikundi hivyo zinaunganishwa pamoja na kuagiza Ng’ombe. “Ng’ombe hawa wametoka Arusha na wanathamani ya shilingi milioni 24. Ni Ng’ombe 12, kwa gharama ya manunuzi mpaka kuwafikisha hapa kila Ng’ombe amegharimu shilingi milioni mbili. Lakini jumla ya fedha ambazo vikundi hivi vimenufaika ni shilingi milioni 44, kwa hiyo bado kila kikundi kina kiasi cha fedha kwa ajili ya chakula, dawa na chanjo” alisema Nabalang’anya.
Kwa upande wa Afisa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi Jiji la Dodoma, Gratian Mwesiga alisema kuwa Ng’ombe wanaogawiwa ni mitamba yenye mimba kati ya miezi sita hadi saba. “Umri wao ni kati ya miezi 18-22. Ng’ombe anauwezo wa kuzaa ndama 10 kwa maana maisha yake ya kuishi ni miaka 10. Hivyo, kila mwaka kama mambo yataenda vizuri atakuwa anazaa ndama mmoja mmoja” alisema Mwesiga. Aidha, alisema kuwa matarajio ya Halmashauri ni vikundi hivyo vifuge Ng’ombe hao kwa miaka 10. Vilevile, aliwataka wanavikundi hao kufuata ushauri wa wataalam wa mifugo ili kuweza kufuga kwa tija.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.