BARAZA la Madiwani wa Manispaa ya Dodoma limemvua madaraka Meya wa Manispaa hiyo Mstahiki Jaffar Mwanyemba kwa tuhuma za matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea upotevu wa shilingi milioni 30 za mradi wa Maji wa Kata ya Zuzu zilizotolewa na Serikali ya Japan kupitia ubalozi wake nchini Tanzania.
Hatua hiyo ilifikiwa katika mkutano wa dharura wa Bazara hilo ulioitishwa jana Aprili tatu katika ukumbi wa Manispaa ili kupokea na kujadili taarifa ya Tume Maalum iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana kuchunguza tuhuma hizo.
Baada ya Katibu wa mkutano huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi kuwasilisha taarifa hiyo, wajumbe waliazimia kupiga kura ya kutokuwa na imani na Meya huyo, ambapo kati ya kura 48 zilizopigwa, kura 43 ziliunga mkono hoja hiyo huku kura 4 zikipinga na moja ikiharibika.
Kufuatia hali hiyo, Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede atakaimu nafasi ya Meya kwa mujibu wa Kanuni katika kipindi cha mpito kisichozidi siku 60, ambapo uchaguzi wa kumpata Meya mpya utafanywa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.