Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia miundombinu Ofisi ya Rais - TAMISEMI Eng. Rogatius Mativila ameongoza kikao cha Menejimenti kurasimisha matumizi ya mfumo wa ujifunzaji Kieletroniki (MUKI)
Mfumo huo umebuniwa na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na kufanyiwa majaribio kwa ufadhili wa Mradi wa USAID wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma Awamu ya Pili (USAID PS3+)
Lengo la mfumo huo ni kuongeza wigo wa kuwafikia walengwawengi wa mafunzo na kupunguza changamoto zinazotokana na utoaji wa mafunzo kwa njia ya ana kwa ana ikiwa pamoja na gharama na muda wa kukamilisha mafunzo hayo kitu kinachosababisha baadhi ya Halmashauri kushindwa kukidhi mahitaji yao ya mafunzo kutokana na ufinyu wa bajeti.
Mfumo huu (MUKI) utatumika sanjari na njia ya ana kwa ana ilikuongeza ubora wa mafunzo yatolewayo kwa viongozi wa kuchaguliwa, Watendaji na Wataalam kwenye Mamlaka zaSerikali za Mitaa na walengwa wengine wa mafunzo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.