MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde (mwenye kaunda suti pichani kulia) leo tarehe 21 Aprili, 2021 amekabidhi saruji tani 29 kwa Afisa Elimu Msingi na Afisa Elimu Sekondari ili kusaidia ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari za Jiji la Dodoma.
Mbunge Mavunde amekabidhi saruji hiyo yenye thamani ya shiling 10,000,000 na kuwataka walimu wakuu na viongozi wa kata husika kusimamia matumizi yake ili kufikia lengo lililokusudiwa.
“Mchango wangu huu ni kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu na hasa katika ujenzi wa madarasa na matundu vya vyoo sambamba na kuunga mkono jitihada za wananchi za ujenzi wa shule mpya za msingi na sekondari, hivyo lazima ninyi viongozi msimamie matumizi sahihi ya saruji hii”,
Nitaendelea kuchangia kwenye sekta hii ya elimu ili kuwafanya wanafunzi wa Dodoma Jiji wasome katika mazingira ambayo ni Rafiki, lakini pia tunaishukuru Serikali kupitia TEA kwa ktupatia shilingi Bilioni 1.9 za ujenzi wa madarasa na majengo ya utawala kwa shule 5 za msingi” amesema Mheshimiwa Mavunde.
Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari wa Jiji la Dodoma, Mwalimu Upendo Rweyemamu amezitaja shule zitakazonufaika na msaada huo kwa upande wa shule za sekondari kuwa ni Mlimwa, Kiwanja cha ndege na shule mpya ya Mkoyo. Kwa upande wa shule za msingi zitakazonufaika, Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Mwalimu Joseph Mabeyo amezitaja kuwa ni shule ya msingi Chinangali na shule mpya za Muungano na Nh'oye.
Nao Madiwani Assedi Ndajilo wa Hombolo Bwawani na Charles Ngh’ambi wa Mbalawala kwa niaba ya wananchi, wamemshukuru Mhe. Mavunde kwa namna anavyochangia maendeleo ya sekta ya elimu kwa kusaidia kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma na wametumia fursa hiyo kuahidi kusimamia vyema matumizi ya saruji hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji, Afisa Elimu Msingi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mabeyo amemshukuru Mhe. Mavunde kwa mchango wake mkubwa kwenye sekta ya elimu kwa namna ambavyo amekuwa akishirikiana na Idara za Elimu Msingi na Sekondari wa Jiji la Dodoma kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde (mwenye Kaunda suti) akijadiliana jambo na Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Mwalimu Upendo Rweyemamu (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi, Mwalimu Joseph Mabeyo (kulia) mara baada ya kuwakabidhi tani 29 za saruji.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.