Mheshimiwa Anthony Mavunde ameongoza wananchi wa Nkulabi, Kata ya Mpunguzi kuanza ujenzi wa Shule ya Sekondari Nkulabi katika kutatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kutoka Nkulabi mpaka Shule ya Sekondari Mpunguzi.
Wananchi wa Mitaa yote ya Nkulabi kwa pamoja waliwasilisha changamoto kwa Mhe. Mavunde ya kukosekana kwa Shule ya Sekondari katika eneo hilo la karibu na hivyo kuomba utatuzi wa kero hiyo ambayo Mavunde alikubali na kuanza utekelezaji wake mara moja.
"Nawashukuru wananchi wote mliojitokeza hapa siku ya leo kwa kujitolea kwenu nguvu kazi na matofali zaidi ya 10,000 kufanikisha kuanza kwa ujenzi wa shule ya Sekondari Nkulabi.
Lazima wananchi tuungane na serikali pamoja na viongozi wetu kujiletea maendeleo yetu wenyewe, ninyi mmekuwa mfano wa wananchi wawajibikaji na ndio maana nimeamua kuwaunga mkono ili malengo yetu yatimie.
Nitagharamia gharama za mafundi zote za kujenga madarasa matatu, na pia nitatoa mifuko 100 ya saruji ili kukamilisha ujenzi huo wa awali." Alisema Mavunde
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wa Nkulabi, Mzee Hudson Mathias Mhepwa amemshukuru Mhe. Mavunde kwa kujitoa kwake kwa wananchi katika kushirikiana kwenye ujenzi wa Sekondari hiyo na kuahidi kuwa nae bega kwa bega mpaka kukamilika kwa ujenzi huo kwa kutoa mchango wa hali na mali.
Mifuko ya saruji aliyochangia Mhe. Anthony Mavunde kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nkulabi katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.