MBUNGE wa Jimboa la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde ametembelea wananchi wa kata ya Msalato ili kuwapa pole na kuwajulia hali kufuatia athari zilizosababishwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo. Nyumba kadhaa zimebomoka na nyingine kuezuliwa mapaa kutokana na upepo mkali.
Baada ya kutembelea maeneo yote yaliyoathiriwa na kuwapa pole wananchi waliopata athari, Mbunge Mhe. Mavunde alitoa msaada wa bati 160 zenye thamani ya Tsh 3,200,000 na Kilo 100 za unga wa sembe.
"Nachukua fursa hii kuwapa pole sana wananchi wote kwa adha hii kubwa iliyopata,nipo hapa kutoa mkono wa pole ili kuwasaidia kurudi ktika hali yenu ya kawaida ya maisha ya kila siku na sasa niwaombe tuchukue tahadhari
Kwa kuwa mvua za sasa hivi kubwa mno hivyo tujitahidi kuwa na tahadhari kubwa"Alisema Mavunde
Akifafanua, Diwani wa Kata ya Msalato Mhe. Ally Mohamed ameeleza kwamba mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali imesababisha kuezuliwa kwa mapaa ya kaya 18, nyumba 4 kubomoka na madarasa 3 ya Shule ya Msingi Msalato kuezuliwa paa.
Baadhi ya Wananchi walioathirika na kupata nafasi ya kuongea mwandishi wetu wamemshukuru Mbunge wao Mhe. Mavunde kwa namna alivyowajali na kuwakimbilia wakati wa matatizo hayo na kuwapa faraja kwa kuwa hatua hiyo imewapa matumaini na faraja na sasa wanaweza kutengeneza na kuzirudisha nyumba zao katika hali ya kawaida wao kuweza kuishi vizuri.
Tazama picha za matukio mbalimbali:
Mheshimiwa Anthony Mavunde (wa pili kutoka kulia) akimsikiliza mmoja wa waathirika wa mvua zilizoambatana na upepo na kusababisha baadhi ya nyumba kuezuliwa mapaa na zingine kubomoka katika kata ya Msalato. Mhe. Mavunde aliambatana na Diwani wa kata ya Msalato Mhe. Ally Mohamed (wa pili kutoka kulia).
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.