Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde amewatembelea wafanyabiashara wadogo wa soko la Sabasaba ambao vibanda vyao viliungua kutokana na ajali ya moto na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa na upotevu wa mali za wafanyabiara zaidi ya 29.
Mhe. Mavunde alitumia fursa hiyo kuwapa pole wafanyabiashara hao kwa janga hilo la moto lililosababisha upotevu mkubwa wa bidhaa zao, ambapo Mbunge huyo amewachangia bati 52 zenye thamani ya Tsh 1,200,000 ili kurejesha vibanda vyao katika hali ya Kawaida.
Naye Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Mh Patrobas Katambi amewataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanapata taarifa za tukio la moto kutoka mamlaka husika kwa ajili ya uthibitisho kwenda Taasisi za fedha ambazo wafanyabiashara hao wamekopa na pia ametumia nafasi hiyo hiyo kuwaagiza TANESCO kutoa elimu ya masuala ya umeme na kuwaunganishia umeme wafanyabiashara hao kwa utaratibu, huku Jeshi la ZIMAMOTO likiagizwa kufika na kutoa ushauri juu ya ujenzi wa vibanda hivyo.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba Jiji la Dodoma litaboresha eneo la Soko la Sabasaba na kujenga vibanda vipya 400 vya kisasa ili soko hilo liendane na hadhi ya Jiji.
Akishukuru kwa niaba,Makamu Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Bi. Eliza Siame amewashukuru viongozi hao kwa kufika eneo la tukio na kuwapa pole pamoja na mchango wa bati 52 ambazo zitasaidia kurejesha vibanda hivyo katika hali yake ya kawaida.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Patrobas Katambi akiongea na wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba alipoambatana na Mbunge Anthony Mavunde na Mkurugenzi wa Jiji Godwin Kunambi.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi akiongea kuwapa wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba na kuwapa mipango na mkakati wa Jiji la Dodoma kuboresha Soko la Sabasaba.
Baadhi ya vibanda vilivyoteketea kwa moto katika Soko la Sabasaba.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.