MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde leo amekabidhi sare maalum kwa kituo cha madereva teksi wa Uwanja wa Ndege Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuboresha hudum ya usafirishaji Jijini Dodoma.
Mhe. Mavunde amekabidhi sare hizo kwa madereva teksi 30 zenye thamani ya shilingi 1,500,000 shughuli iliyofanyika katika eneo la Uwanja wa Ndege lengo ikiwa ni kuwafanya madereva hao kuwa nadhifu na kuwatambulisha kwa urahisi kwa wageni waingiao Dodoma kupitia Kiwanja hicho cha Ndege.
“Kwa kuwa ninyi mnapokea wageni kutoka maeneo mengi tofauti nchini na duniani, ni vema mkawa na utambulisho mzuri kupitia sare hizi na pia kuwa nadhifu muda wote ili wageni waingiao wapate sura halisi Jiji la Dodoma kupitia ninyi”,
Dodoma sasa ni Makao Makuu ya nchi, yatupasa kuboresha huduma hizi za usafiri kwa kuonesha utofauti na maeneo mengine kwa kuanzia kwenye unadhifu wa mavazi mpaka ukarimu kwa wageni wetu,
Baada ya kumaliza suala hili la sare, najiandaa kuratibu semina kwa ajili ya mafunzo ya ukarimu kwa watoa huduma mbalimbali katika Jiji la Dodoma mkiwemo nyingi wa sekta ya usafirishaji, lengo langu ni kuona huduma mbalimbali Jijini Dodoma zinaenda na kasi ya ukuaji wa Jiji na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii” amesema Mbunge Mavunde.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Teksi wa Uwanja wa Ndege Dodoma, Lotson Mushobozi Nkongo kwa niaba ya madereva teksi wenzake, amemshukuru Mbunge Mhe. Mavunde kwa kuwajali watoa huduma ya usafiri katika kituo cha Uwanja wa Ndege kwa kuwapa sare nadhifu ambazo zitawatambulisha vyema kwa wageni na kuahidi kuitangaza vyema Dodoma na kutoa huduma bora kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kulinda sifa ya Makao Makuu ya Nchi Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.