Mbunge wa Dodoma Mjini mhe. Anthony Mavunde ametimiza ahadi yake ya kufikisha nishati ya umeme katika Zahanati ya Nkulabi Kata ya Mpunguzi na hivyo kusaidia upatikanaji wa huduma ya afya kwa saa 24 katika zahanati hiyo.
Mavunde amefanikisha upatikanaji wa nguzo saba za umeme zenye gharama ya shilingi 9,698,876 na malipo ya kuunganishiwa umeme zahanati hapo, jambo ambalo limepokelewa kwa furaha kubwa sana na wananchi wa eneo hilo la Nkulabi Kata ya Mpunguzi.
"Leo (23 Juni, 2020) ni siku ya kihistoria katika utoaji wa huduma za afya katka kata yetu, kuanzia leo tutashuhudia upatikanaji wa huduma za afya mpaka usiku tofauti na zamani ambapo mlikuwa mnapata taabu kupata huduma ifikapo usiku.
Niwaombe wahudumu wote wa afya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kwa ufanisi na maadili mema kwa muda wote na kwasasa kwakuwa mna umeme natarajia kuona uboreshwaji mkubwa sana wa huduma hii muhimu kwa wananchi," alisema Mavunde.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi waliojitokeza katika viwanja hivyoa vya zahanati, Mzee Steven Myeya amemshukuru Mheshimiwa Mavunde kwa kazi kubwa aliyoifanya kwenye sekta ya afya kwa kufanikisha umeme ambao utawafanya sasa wapate huduma ya uhakika kwa muda wote.
Wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi Kata ya Mpunguzi kimemshukuru Mhe. Mavunde kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika utatuzi wa kero za wananchi na kwa hatua yake ya kuamua kutoa saruji mifuko 50, mbao na mabati 100 ili kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi na pia kukubali kuanzisha mchakato wa ujenzi wa Shule ya Sekondari katika eneo la Nkulabi.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akiwa pamoja na watumishi, viongozi na wananchi wa Nkulabi wakifurahia umeme ambao umeanza kutumia katika Zahanati ya Nkubali katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.