MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ameahidi kufanikisha ujenzi wa uzio wa Shule ya Sekondari Dodoma kwa lengo la kuongeza ulinzi kwa wanafunzi na mali za shule.
Mbunge Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya mahafali ya kidato cha IV shuleni hapo kufuatia maombi yaliyowasilishwa na wanafunzi kupitia risala iliyosomwa mbele yake.
“Nataka niwahakikishie kwamba tutamalizia ujenzi wa eneo la uzio lililobaki ili kulizungushia eneo lote la shule na uzio kwa madhumuni ya usalama wa wanafunzi na mali zote zilizopo shuleni.
Tunashukuru kazi kubwa iliyofanywa na wanafunzi waliosoma hapa wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndg. Masanja Kadogosa kwa ujenzi wa uzio kwa awamu ya kwanza, nawahakikishia kwamba tutamalizia palipobaki.
Lakini pia kipekee niishukuru sana serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuingiza kiasi cha Tsh 60,000,000 za ujenzi wa madarasa matatu ambayo yatasaidia sana kupunguza changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa” Alisema Mavunde.
Akitoa maelezo ya awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Dodoma Mwl. Aman Mfaume amebainisha mikakati ya kitaaluma ambayo shule imejiwekea ikiwa ni pamoja na kuwa na masomo ya ziada (remedial classes) ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wananafanya vizuri katika mitihani ya Taifa na hivyo kuijengea sifa wilaya ya Dodoma Mjini na mkoa kwa ujumla.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.