Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde aahidi kutoa shilingi 2,000,000 kwa timu ya Mkoa wa Dodoma inayoshiriki mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za Msingi na Sekondari (UMITASHUMTA na UMISSETA) iwapo watashinda makombe Matano kwenye mashindano yatakayoanza mkoani Mtwara wiki ijayo.
Kauli hiyo ameitoa leo katika hafla fupi ya kuwatakia heri wanamichezo hao na kugawa “tracksuit” 100 kwa wanamichezo wanaounda timu ya mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) katika shule ya Dodoma sekondari jijini hapa.
Mbunge Mavunde amesema “nichukue nafasi hii kuwapongeza wanamichezo wote mliochaguliwa kuuwakilisha Mkoa wa Dodoma katika mashindano ya UMITASHUMTA. Najua mmefanya mazoezi ya kutosha. Nendeni mkoani Mtwara mkalilinde na kulitetea jina la Dodoma. Sisi tunaobaki tutawaunga mkono katika kila hatua mtakayopitia”.
Adha, Mbunge huyo aliwataka kuwa na nidhamu katika kipindi chote cha mashindano hayo. “Mtakapokuwa mkoani Mtwara muishi kwa nidhamu katika kipindi chote. Nawaahidi mkishinda makombe matano, nitawapatia zawadi ya shilingi 2,000,000. Nawatakia kila la heri na Mungu awaongoze” amesema Mbunge Mavunde.
Awali, Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwalimu Upendo Rwenyemamu alimpongeza mbunge huyo kwa utayari wake katika kuendeleza sekta ya elimu jijini hapo. “Mheshimiwa Mbunge tunayofuraha kuwa nawe hapa. Tunakushukuru kwa utayari wako wa kutuunga mkono si katika michezo pekee, bali katika elimu kwa ujumla. Mchango wako ni mkubwa katika kukuza taaluma Jiji la Dodoma” amesema Mwalimu Rweyemamu.
Kwa upande wake, mshiriki wa michezo ya UMITASHUMTA Mkoa wa Dodoma, Nasri Dismas amesema kuwa matarajio yake ni timu ya Mkoa wa Dodoma kuleta makombe mengi. “Sisi wachezaji tutaonesha vipaji katika michezo yote tutakayoshiriki na kupata ushindi” amesema Dismas.
Timu ya UMITASHUMTA Mkoa wa Dodoma inatarajia kuondoka kesho Jumamosi kuelekea mkoani Mtwara kushiriki michuano hiyo.
Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwalimu Upendo Rweyemamu alipokuwa akimshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde kwa msaada mkubwa anaoutoa kuchangia maendeleo ya elimu Jijini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi watakaoshiriki michezo ya UMISSETA kuwakilisha mkoa wa Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.