Aliyekuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mhe. Jumanne Ngede amefanikiwa kutetea kiti hicho katika uchaguzi wa uliofanyika Agosti Mosi, 2018 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini humo.
Mhe. Ngede ambaye ni Diwani wa Kata ya Chamwino kupiti Chama cha Mapinduzi (CCM), aliibuka mshindi kwa kupata kura 48 za ndiyo dhidi ya mpinzani wake Mhe. Vicent Thibalinda wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura 7.
Mgombea aliyeshinda nafasi ya Naibu Meya wa Jiji la Dodoma Jumanne Ngede (CCM) akitoa neno kwa wajumbe mara baada ya kushinda nafasi hiyo kufuatia uchaguzi uliofanyika mwaka jana katika ukumbi wa Jiji, ambapo ametetea tena nafasi hiyo mwaka huu wa 2018. Wa pili kushoto ni Meya wa Jiji la Dodoma Mstahiki Profesa George Mwamfupe na kwanza kushoto ni Mkurugenzi Godwin Kunambi. PICHA-Maktaba Ofisi ya Mkurugenzi.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ambaye ni Katibu wa Baraza la Madiwani na Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Mjini alimtangaza rasmi Mhe. Ngede kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji hilo.
Baada ya kufanikiwa kutetea nafasi hiyo, Mhe. Ngede aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua kwa kura nyingi jambo linaloonesha kuwa wana imani kubwa na utendaji wake na kwamba ataendelea kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kwa kushirikiana na Madiwani wote.
Katika uchaguzi huo, jumla ya wajumbe 56 kati ya 60 wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo walipiga kura, huku kura moja ikiharibika ambapo sasa Mhe. Ngede anaungana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mhe. Profesa Davis Mwamfupe kuongoza Baraza hilo la Madiwani.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.