Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli ameupandisha hadi Mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji, na amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mhe. Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo tarehe 26 Aprili, 2018 wakati akihutubia katika sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanzanyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Pamoja na kupandishwa hadhi Mji wa Dodoma Mhe. Rais Magufuli ameagiza taratibu za kisheria zifanyike kukamilisha mchakato huo, na amesisitiza kuwa azma ya Serikali kuhamia Dodoma inaendelea kutekelezwa na yeye mwenyewe atahamia mwaka huu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.