RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameanza kusuka Baraza lake la Mawaziri baada ya leo Novemba 12, 2020 kuteua Mawaziri wawili ikiwa ni saa chache kabla ya kuhutubia taifa kupitia Bunge la 12 na kulizindua rasmi Novemba 13, 2020 Jijini Dodoma.
Mawaziri walioteuliwa ni Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Dkt. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
Mawaziri wateule hao walikuwa wakishikilia nyadhifa hizo kwenye Baraza la Mawaziri lililopita na uteuzi huo unaanza rasmi leo Novemba 13, 2020.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.