• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mhe. Rais Magufuli aweka jiwe la msingi ujenzi wa mahandaki 4 Kilosa

Imewekwa tarehe: June 29th, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Juni, 2020 ameweja jiwe la msingi la ujenzi wa mahandaki 4 ya milima inamopita reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge) likiwemo handaki refu kuliko yote nchini na ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Kilosa-Rudewa Mkoani Morogoro.

Sherehe za uwekaji jiwe la msingi la miradi hiyo miwili zimefanyika katika eneo la Mkadage Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, lilipojengwa handaki lenye urefu wa kilometa 1.1 ambalo linakua handaki la reli refu kuliko yote hapa nchini na ni moja ya mahandaki 4 yenye jumla ya urefu wa kilometa 2.7 katika mradi wa ujenzi wa reli hiyo kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupola Mkoani Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mawaziri, Makatibu Wakuu, viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakandarasi na Wakuu wa Mikoa ya Morogoro na Dodoma amelikagua handaki hilo kwa kutembea na miguu umbali wa zaidi ya kilometa 1 na ametia saini katika ukuta wa lango la handaki hilo.

Mahandaki hayo yanachimbwa ili kuwezeshas treni kukwepa milima na mito ukiwemo mto Mkondoa ulio kando ya handaki refu la Mkadage ambalo litaunganishwa na daraja refu meta 487 la kuvuka mto huo.

Barabara iliyowekwa jiwe la msingi ni ya Kilosa - Rudewa yenye urefu wa kilometa 24 ambayo ujenzi wake unafanywa na muungano wa kampuni za ukandarasi za Tanzania kwa gharama ya shilingi Bilioni 33.4. Barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Dumila - Kilosa - Mikumi ambayo inapita nje ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na katika maeneo ya uzalishaji wa mazao.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mkadage, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na kazi nzuri ya utoboaji wa milima ili kupata mahandaki hayo, lakini ameelezea kutofurahishwa na ujenzi wa barabara ya Kilosa - Rudewa na hivyo ametoa mwezi mmoja kwa kazi hiyo kuanza kwa kasi inayotakiwa, vinginevyo wakandarasi  watafukuzwa na viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano watawajibishwa.

Amewataka Watanzania wote kutembea kifua mbele kwa mafanikio makubwa ya ujenzi wa reli ya kati kwa sehemu ya kuanzia Dar es Salaam - Morogoro - Makutupora ambayo ujenzi wake utagharimu shilingi Trilioni 7.026 na miradi mingine mikubwa ukiwemo Bwawa la Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 kwa gharama ya zaidi ya shilingi Trilioni 6 na kuhamisha Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Makao Mkuu Dodoma kwa kuwa miradi  hiyo inatekelezwa kwa fedha za Watanzania wenyewe.

Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania hasa waliopo  karibu na maeneo ya utekelezaji wa miradi hiyo  kuchangamkia fursa mbalimbali za kujipatia kipato na kuongeza uzalishaji mali ikiwemo kulima mazao na kuanzisha shoroba za uzalishaji.

Kuhusu  maombi ya ujenzi wa barabara la lami, Mhe. Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya lami ya Kilosa - Mikumi yenye urefu wa kilometa 70 na barabara ya Ifakara - Malinyi - Londo.

Akiwa njiani kuelekea Mkadage, Mhe. Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Kijiji cha Kimamba ambao wamelalamikia kitendo cha mwekezaji ambaye sio raia wa Tanzania kumilikishwa shamba la ekari 5,000 kinyume na sheria ilihali wao wanakosa mashamba ya kulima.

Na akiwa njiani kutoka Mkadege , Mhe. Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Kijiji cha Ilonga Wilayani Kilosa ambao wamelalamikia kitendo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bw. Asajile Mwambambale kuidhinisha mwekezaji Swai Frank Palilo aachiwe shamba lenye ukubwa wa ekari 1,200 hata kabla Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi hajatoa maamuzi baada ya timu aliyounda kudhughulikia mgogoro huo kuwasilisha ripoti ya uchunguzi kwake.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewaonya viongozi wa Wilaya ya Kilosa kwa kutoshughulikia kero mbalimbali za wananchi ipasavyo hususani migogoro ya ardhi, akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ambaye amemuomba Mhe. Rais na wananchi wa Kijiji cha Ilonga kwa kuidhinisha shamba kubwa apatiwe mwekezaji mmoja ilihali wananchi wanakosa mahali pa kulima.

Mhe. Rais Magufuli amerejea Chamwino Mkoani Dodoma akitokea Mkoani Morogoro alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku 2.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na baadhi wa Mawaziri , Wakuu wa Mikoa, viongozi mbalimbali, akikata utepe ili kuzindua mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Reli ya kisasa SGR katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro.

Rais Mhe. Dkt. John Magufuli akipita ndani ya handaki kubwa lenye urefu wa kilometa 1.1 kulikagua mara baada ya kuweka jiwe la msingi la miradi hiyo ya ujenzi Kilosa mkoani Morogoro.



Rais Mhe. Dkt. John Magufuli akifurahia jambo wakati akitoka kwenye handaki kubwa la Reli ya Kisasa mara baada ya kulikagua.

Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Ujenzi Mhandisi Isack Kamwelwe wakati akionesha sehemu litakapojengwa daraja la kupitisha Reli katika Mto Mkondoa  Kilosa mkoani Morogoro.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.