MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amefanya ziara ya kikazi kukagua Mradi wa Kituo Mahiri cha usimamizi wa mazao ya nafaka Katika Kata ya Mtanana, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Akiwa kwenye ziara hiyo Mhe. Senyamule amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mtu wa vitendo zaidi na wengi wanamtafsiri kwa namna hiyo na uthibitisho unaonekana katika miradi iliyoletwa kwenye Mkoa wa Dodoma.
“Mhe. Rais anataka kuanzia shambani hadi kwenye bidhaa ya mwisho ameshaitengenezea mkakati wake. Tunaona analeta Mabwawa makubwa katika Mkoa wetu ambayo yanagharama kubwa sana ili wananchi wake waweze kunufaika na Kilimo cha umwagiliaji kwa mwaka mzima.“Kituo hiki kitafanya kazi kwa kupima kama mazao yana Sifa ambazo maafisa kilimo wanaridhika nazo, kupimwa ubora na kuhakikisha kuwa unyevu wake unaweza ukamudu au kudumu kwa muda mrefu kusafirishwa nje ya nchi.
Vile vile, RC Senyamule amekagua Miundombinu ya Soko, kiwanda cha kusindika nafaka na kituo cha uhaulishaji wa teknolojia.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi huo Bw.Clepin Josephat, amesema utekelezaji wa Mradi huo utakamilika kwa mujibu wa Mkataba na kwa ubora stahiki na Serikali kupata thamani ya fedha tarajiwa kwa kuhakikisha afua zote za Mradi wa TANIPAC uliogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 18 zinazingatiwa
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.