Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema Mifuko ya Pensheni nchini imeweka utaratibu wa kuhakiki wastaafu kwa kutumia mifumo ya TEHAMA.
Aidha, Mhe. Katambi amesema Mifumo ya uhakiki wa wastaafu kwa kutumia alama za vidole (Biometric Verification) imesaidia zoezi la uhakiki kwa wastaafu kufanyika kwa urahisi.
Ameyasema hayo bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge, Mhe. Maimuna Pathan ambaye ametaka kufahamu kwa nini Serikali isifanye utaratibu wa kwenda kuhakiki wastaafu kwenye wilaya zao kuliko ilivyo sasa kuhakikiwa mikoani.
Kwa upande wengine, Mhe. Katambi amesema Serikali itaendelea kusimamia maboresho katika utoaji wa huduma kwa wastaafu ili kupunguza changamoto za kusafiri umbali mrefu na kuwapunguzia gharama zisizo na lazima.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.