HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imezindua Mpango Mkakati wa kusikiliza, kuorodhesha, na kutatua kero zote za ardhi katika Kata zote 41 za Jiji hilo.
Zoezi hilo limezinduliwa rasmi na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi leo Oktoba 5, 2018, katika Kata ya Kikuyu Kusini ambapo alizungumza na Wakazi wa Kata hiyo na kuahidi kuwa Halmashauri itashughulikia migogoro hiyo kwa haki kwa kuongozwa na nyaraka mbalimbali zilizopo kwenye Ofisi ya Halmashauri ya Jiji na zile za wamiliki wa maeneo hayo.
Mkurugenzi huyo alizindua zoezi hilo kwa kusikiliza kupokea kero kadhaa za Wananchi kabla ya kuwaacha wataalam wa ardhi wa Jiji kuendelea na kazi hiyo.
“Wataalam wa Ardhi na Mipango Miji watakuwa hapa kwenye Kata yenu kwa muda wa siku nne kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni…hata mtu aliyesafiri anaweza kurudi na kuwasilisha kero yake ndani siku hizi nne” alisisitiza Kunambi.
Baadhi ya wakazi wa Kata hiyo waliezea kufurahishwa kwao na ujio wa Mpango huo huku wakimshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kwani wanaamini kwa utaratibu huo kero zao zitapata ufumbuzi.
Baada ya zoezi hilo kuzinduliwa katika Kata ya Kikuyu Kusini leo, litendelea katika Kata zingine 40 zilizobaki ili kuhakikisha kila Mwananchi mwenye kero anasikilizwa na kero husika kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.