Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika kipindi cha Julai-Septemba, 2022 tukio lililofanyika katika bustani ya mapumziko ya Chinangali iliyopo katikati ya Jiji la Dodoma.
Mkurugenzi Mafuru alisema kuwa katika kipindi cha Julai-Septemba, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipokea maombi ya mikopo yenye thamani ya shilingi 5,813,813,500 kutoka kwa vikundi 198 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. “Baada ya uchambuzi, jumla ya vikundi 102 viliidhinishwa kupewa mikopo yenye thamani ya shilingi 1,389,552,700 ambapo vikundi 46 vya wanawake vimekopeshwa shilingi 501,000,000, vikundi 33 vya vijana vimekopeshwa shilingi 693,294,100 na vikundi 23 vya watu wenye ulemavu vimekopeshwa shilingi 195,258,600” alisema Mkurugenzi Mafuru.
Akiongelea mchanganuo wa fedha hizo, alisema kuwa fedha hizo ni mchango wa halmashauri na marejesho. “Kati ya fedha zilizokopeshwa kwa vikundi, shilingi 467,481,558.41 ni mchango wa halmashauri wa asilimia 10 wa mapato ya ndani na shilingi 922,071,141.59 ni fedha za marejesho. Vikundi hivi vitaanza kufanya marejesho mwenzi Februari, 2023” alisema Mkurugenzi Mafuru.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.