Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MIRADI ya maendeleo inayotekelezwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeanza kutoa matunda kwa jiji hilo na kuchangia katika utoaji huduma bora kwa wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Halmasahuri ya Jiji la Dodoma, Francis Kaunda alipokuwa akiongelea mafanikio ya miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka miwili ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Sulihu Hassan.Kaunda alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa mapato ya ndani ya halmashauri.
Mradi wa ujenzi wa hoteli ya Jiji la Dodoma (Dodoma CityHotel) umegharimu shilingi 11,945,995,952.50 ambazo ni mapato ya ndani ya halmashauri. Jengo hilo lina ghorofa11, ikijumuisha vyumba 95 vya kulala, kumbi tatu za mikutano, mgahawa na bwawa la kuogelea katika ghorofa ya mwisho. Mradi unaingizia Halmashauri kiasi cha shilingi 600,000,000 kwa mwaka alisema Kaunda.
Akiongelea mradi wa jengo la kitega uchumi cha Jiji laDodoma (Government City Complex - Mtumba) alisema kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi18,875,665,009.83.
Jengo la Hoteli lina ghorofa sita pamoja na maeneo ya maduka na sehemu ya kutolea huduma za fedha. Mradiuna kumbi za mikutano saba. Ukumbi mmoja mkubwa wenye uwezo wa kuchukua watu 1,000 na kumbi ndogo sita zenye uwezo wa kuchukua watu 80 hadi 100 kila moja.
Hadi sasa mradi umeingiza shilingi 432,628,048. Akifafanua kuhusu mapato yatokanayo na miradi hiyo ya maendeleo, alisema kuwa fedha hizo zinakwenda kuboresha huduma za kijamii katika jiji hilo.
Mradi huo unategemea kuiingizia Halmashauri kiasi cha shilingi1,999,128,048.00 kwa mwaka.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.